Monday, 25 July 2016
Harmmer q kuachia mkwaju wake mpya kabisa leo Tue,july 26
Msaniii wa miondoka ya style nyingi ikiwemo Bongo fleva ,Mduara hata zile za Arabik style Kwa jina anajulikana Hammer q leo kachia kibao chake kipya kabisa chenye style ya tofaut na ngoma zake zote . Anahitaj sapport ya kutosha kutoka kwenu mashabiki - ngoma inaitwa Hatotokea by Hammer Q
Thursday, 9 June 2016
Zlatan Ibramovich huwenda akawa Star wa tatu kusajiliwa na JoseMorinyo
Baada ya jana June 8 klabu ya Man United iliyopo chini ya Jose Mourinho kufanikiwa kufanya usajili wake wa kwanza kwa kunasa saini ya Eric Bailly kutoka Villerreal ya Hispania, leo June 9 2016 wameripotiwa kutenga kiasi cha pound milioni 47 ambazo ni zaidi ya bilioni 140 za kitanzania kwa ajili ya kuishawishi Juventus ya Italia iwauzie Alvaro Morata.
Tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa na wengi kuwa Zlatan Ibrahimovic ndio staa atakayefuatiwa kusajiliwa Man United baada ya Eric Bailly, lakini taarifa zimetoka kuwa Man United wanalazimika kuchelewesha usajili wa Zlatan hadi June 31 ili amalize mkataba wake rasmi na PSG, kwani akisaini wakati huu atalazimika kuilipa PSG kutokana na mkataba wake kuwa na kipengele cha uaminifu.
Monday, 9 May 2016
Dar es salaam Nauli za mabasi yaendayo kasi zatajwa
Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni tsh 650 na mwanafunzi 200.
Njia kuu+pembezoni nauli ni 800 na mwanafunzi 200 mfano njia kuu yaani kutoka Kimara mpaka kivukoni nauli itakuwa 650 na ukitoka mbezi mwisho mpaka kivukoni (hapo umechukua njia ya pembeni ukaunganisha na njia kuu) nauli itakua 800, ukitoka Morroco mpaka kariakoo au kivukoni nauli itakuwa 650 mwanafunzi 200.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.
Msimamizi wa mradi kutoka DART, Eng Ronald Lwakatare amesema……….>>>‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’
Thursday, 5 May 2016
About Me
kwa ufupi jina langu kamili Lukman soud Almas blog hii ni mali yngu ambayo namiliki takriban miez 3 bado mpya. Nahitaj saport sna kutoka kwenu kwani bila nyie kufatilia habari toka kwa hii blog itakuwa si chochote kwangu. Naombeni saport ili tuweze fika mbali.
INSTAGRAM NATUMIA bizyluqdube
FACEBOOK bizyluq
TWITER bizyluqd
Wednesday, 4 May 2016
Mambo matatu aliongea Ronado baada mchezo kumaliza na kutinga Final UEFA
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa siku 15 bila kucheza mechi yoyote ya ushindani kwa Cristiano Ronaldo, Usiku wa May 4 2016 aliingia kwenye headlines baada ya kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Man City akitokea majeruhi na kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Ronaldo alinaswa katika interview baada ya mechi kumalizika lakini amekaririwa akiongelea mchezo na kueleza kuwa wao walicheza vizuri kuliko Man City, walitengeneza nafasi nyingi kuliko Man City, kuhusu majeruhi alisema anashangaa kwa watu wenye mashaka na fitnes yake kwani yeye yupo fiti.
“Ulikuwa ni mchezo mgumu lakini nafikiria kuwa tulicheza vizuri zaidi ya Man City, licha ya kutotumia nafasi tulitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza na cha pili, kuhusu majeruhi mimi nipo sawa japokuwa watu wana mashaka na fitness yangu sijui kwa nini, fainali ya UEFA natoa aslimia 50 kwa 50 kwetu sisi kushinda au Atletico”
Uteuzi mwengine wa Rais Magufuli
Taarifa kutoka Ikulu May 04 2016 imeeleza kuhusu uteuzi alioufanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, Rais Magufuli amemteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dododoma
Monday, 2 May 2016
Baada ya Daraja la kigamboni kuanza kutumika watumiaji wategemee hili
April 16 2016 ni siku ambayo wakazi wa kigamboni walianza kulitumia daraja la ‘Nyerere’ Kigamboni na baaadae Daraja la Nyerere ‘kigamboni’ lilifunguliwa rasmi April 19 2016 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John pombe Magufuli.
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) David Mziray ameongelea uanzishwaji wa usafirishaji wa abiria kwa daladala kupitia daraja la Nyerere ‘Kigamboni’ Dar es salaam…
>>>‘tunaomba kuamasisha wamiliki wa mabasi kuja kupata leseni kwa ajili ya kutoa huduma ya Kigamboni kwenda mbagala rangitatu, kigamboni kwenda temeke, kigamboni- stesheni, sasa hivi njia hizo ziko wazi, tunaamasisha magari ambayo yanabeba abiria 27 na kuendelea, nauli zinaanzia 400 mpaka 450‘
Swansea yaichapa Liverpool
Swansea City imeitoa nishai Liverpool na kujihakikishia maisha kwenye Premier League ndani ya msimu ujao.
Andre Ayew alianza kutupia bao la kwanza kwa kichwa kabla ya goli linguine kutoka kwa Jack Cork na kuiweka Swansea mbele kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0.
Goli la Christian Benteke ililifufua matumani kwa Liverpool kipindi cha pili lakini la pili la Andre Ayew ambalo lilikuwa ni la tatu kwa upande wa Swansea lilimaliza matumaini ya Liverpool japo kuondoka na pointi moja kutoka uwanja wa ugenini.
Brad Smith kwa upane wa Liverpool alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano.
Matumaini ya Liverpool kufuzu kucheza Champions League yamebaki kuwa ni kutwaa taji la Europa League pekee.
Ushindi huo unamaana kubwa kwaSwansea ambao wamebakiza michezo miwili tu kabla ya ligi kumalizika, matokeo hayo yanawafanya wasalie nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi huku wakiweka gap la pointi 11 kati yao na Sunderland inayoshika nafasi ya tatu kutoka chini.
Mambo muhimu ya kufahamu
Andre Ayew amefunga magoli mawili kwenye mechi moja kwa mara ya kwanza tangu atue Swansea.Swansea imefurahia ushindi wake wanne mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwenye Premier League.Christian Benteke amefunga goli lake la 50 ndani ya Premier League.Swansea imefunga magoli matatu kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho 25 April, 2015, time Jack Cork kwa mara ya mwisho.Gylfi Sigurdssonamehusika kwenye magoli 41 ya Swansea ndani ya Premier League (amefunga magoli 25 na kutoa assists 16), magoli 10 zaidi ya mchezaji yeyote wa Swansea (Wilfried Bony ndiye anayefata akiwa kahusika kwenye magoli 31 wakati akiitumika klabu hiyo).
Mzee Majuto atangaza rasmi kusataafu Kuigiza
Siku ya kwanza ya May 2016 jina la Mzee Majuto limetajwa tena kwenye vichwa vya habari kuhusu kuacha kwake kuigiza,
Gwiji la sanaa ya maigizo nchini Amri Athmani aka Mzee Majuto ametangaza rasmi kustaafu kuigiza na kutumia muda wake kumtumikia mola wake. Majuto amekuwa akifanya sanaa hii ya maigizo kwa muda mrefu na alianza kupata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 90.
Nisha sishtuki na head lines na sijawahi kuwa na Baraka
Jina la kuzaliwa Salma Jabu ila umaarufu anajulikana kwa jina la Nisha. exclusive
Kuna ripoti ziliandikwa kwamba ulikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji Baraka Da Prince na ukasema humjui kabisa? JIBU >>> ‘Sijawahi kuandika hicho kitu na huwa simuandiki mtu kwenye page yangu, sipendi kuhusisha maisha yangu binafsi na maswala ya kazi yangu kwenye mitandao, sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, wa kirafiki au wa aina yoyote na Baraka Da Prince’
Umeshawahi kuwazia chochote kuhusu spidi ndogo ya Bongo movie kwenda nje ya mipaka ya Tanzania?
JIBU >>> ‘Mimi na timu yangu tulikaa tukalitazama hilo pia kama unakumbuka miezi miwili iliyopita kuna picha ziliruka nikiwa na mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi, kuna kitu kikubwa kinakuja kitahusisha soko la Afrika Mashariki‘
Sasa hivi una umri wa miaka 27, una mtoto tayari?
JIBU >>> ‘Ninae mtoto wa kike ana umri wa miaka 11, nilimpata nikiwa na miaka 17…. mitihani ya kidunia inatokea kila mtu ana historia yake, nilijutia lakini unaizoea ile hali na kujifunza kupitia ulipokosea… ni stori ya kusikitisha na nikiiongea itaniumiza nitaanza kulia lakini ni kitu kiliniathiri sana kisaikolojia’
wanawake muwe makini huyu inasadikika kafa gest jana Amelishwa sumu
Tukio limetokea Guest House Kimara Dar es salaam usiku wa May 1 2016 ambapo Mwanaume mmoja aliyeingia kwenye nyumba hiyo ya Wageni akiwa na Mwanamke, alikimbia kwa kusingizia kwenda dukani kununua vocha wakati Mwanamke huyo akikaribia kukata roho na hakurudi tena.
Wakati tunasubiri uchunguzi wa Polisi, mashuhuda kwenye eneo la tukio wamesema inavyoonekana Mwanamke huyo atakua kawekewa sumu kwenye chips alizokua anakula ndani ya chumba cha nyumba hiyo ya Wageni chips ambazo inadaiwa walitokanazo kwenye safari yao na kuja nazo Guest House.
Sunday, 1 May 2016
Nakupa Kikosi cha simba zidi ya Azam Leo hii May1 2016
1.Vicent Agban
2.Emery Nimuboma
3.Mohammedi Tshabalala
4.Juuko Murshid
5.Novart Lufunga
6.Justise Majabvi
7.Awadh Juma
8.Jonas Mkude
9.Hamis kiza
10.Dany Lyanga
11.peter Mwalyanzi
Bench.
Peter Manyika
Mohammedi Fakhi
Hassani Is-haka
Brian Majwega
Mussa Mgosi
Harmonize kufanya balaa Geita jana April30 2016
Domayo aikosa Simba Kipre arejea.
kwa ufupi
Kiungo wa Azam Frank Domayo ataendele kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili kutokana na maumivu ya cha mguu, Lakini mshambuliaji Kipre ypo fiti kuivaa Simba leo
Memphis Depay aondoka Man United
winga mshambuliaji wa klabu ya Man united ya uingereza Memphis Depay jina lake limeingia kwenye headlines tena baada kufanya kitendo ambacho huwenda kikawa na maana ya kuwashiria yeye kukosa furaha ndani ya Man united .Memphis amewashangaza wengi hususani mashabiki wake wa Man United wanao Mfollow katika acout yake ya Instagram baada kuona wingi hyo kufuta picha zote zinazo husu Man United ambazo aliwah ku post.
Jambazi sugu lakamatwa Posta wawili wakimbia....Noah yakamatwa
Kijana mmoja anae sadikika jambazi akamatwa jijini Dar se salaam maeneo ya posta ,baada kutaka kumtapeli mama mmoja anae fanya kazi tigo pesa. Mashahidi waliokuwepo kwenye eneo hilo wanasema alikuwa analengo la kutaka kuweka pesa kiasi cha shilingi elf5. wakati yule dada anahesabu pesa zake kwanza ndipo yule jambazi akakwapua na kukimbia kwenye gari aina ya Noah, na kumrushia mtu alie kuwepo nyuma ya hilo gari. Wakati mchezo unaendelea dereva akajianda kuwasha gari ndipo raia wakamchomoa dereva na kumpiga na yule alieiba pesa wakamkamata . kama unavyo ona kwenye pcha
Saturday, 30 April 2016
Mbunge Prof. Anna Tibaijuka amtaka Raisi Magufuli ache kutumbua nyama akizani ni majipu
Amesema "naafiki kuanzishwa mahakama ya mafisadi.labda itasaidia kukamatwa na kushtakiwa mafisadi wenyewe.labda zitaachwa kukamuliwa nyama zikizaniwa majipu. Alisema Prof Tibaijuka
Morinyo kudondoka Man United
Baada ya kimya kingi wiki hii anatarajia kuachia ngoma mpya
Msaniii alietamba na ngoma ya Shikolobo (shetta) ndani ya wiki hii anatarajia kuachia New single Kabisa chini ya usimamizi wa Johbanjo studio. Wimbo huo utajulikana kwa jina la NAMJUA
Barcelona yakabiliwa na upinzani mzito
Klabu ya barcelona italazimika kishinda mechi zake zote za mwisho ili kishinda taji la Laliga kwa kuwa huwenda wapinzani wao wasipoteze point hata moja kulingana na kocha Kuis Enrique
Furaha ya ushindi wa Yanga leo April 30 /2016
Leo Yanga ilikuwa uwanja wa ccm kilumba mwanza kucheza mchezo wao wa 26 wa ligi kuu ya Tanzania bara zidi ya wenyeji wao Toto African. Na Yanga kuibuka kidedea kwa magoli 2 kwa 1
Breaking news Jengo lenye ghorofa sita katika mji wa Nairobi laporomoka na kusababisha vifo
Mvua zinazoendelea kunyesha mjini Nairobi zimesababisha vifo vya watu wapatao 15 baada ya Jengo la ghorofa kuporomoka na kati yao 7 wamefariki baada Jengo kuwaporomokea usiku wa Ijumaa katika eneo la khuruma na zaidi ya watu 120 wameokolewa.
Baada ya tetesi za usaliti Beyonce na Jay z Bado wanacheka pamoja
Hivi karibuni kulikuwa na story kibao Kuhusu usaliti uliofanywa na Jay Z na mwanamke ambaye alie tajwa kwa jina la Beck kwenye wimbo wa Sory wa beyonce. Hivi karibuni katika show ya Miami ya beyonce. Jay alionekana kuwa na mwanamke wake bila kusumbuliwa kabisa na story zinazoendelea juu yake.
Diamond na meneja wake hakuwa nyuma leo kwenye kampen ya usafi
Breaking news Abiria wanusurika na ajali ya ndege hii leo mjini Bukoba
Watu kadhaa wanusurika baada ya shirika la ndege Auric Air waliokuwa wakisafiria kupata ajali katika uwanja wa ndege manispaa ya Bukoba. Ndege hio ilipata pancha tayair ya nyuma upande wa kulia ilipo kuwa inatuwa , kwa umahir wa rubani ameweza kuicontrow kama unavyo ona kwenye picha. Ndege hio ilikuwa ikisafiri toka jiji mwanza tukio hilo limetokea leoo majira ya saa4 asubuh April 30-2016
Mengi yalioandikwa kuhuhusu Morinyo
Bado headlines za kocha wa sasa wa Man united Luois Van Gaal kutimuliwa ndan ya Man united na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Morinyo, zinazidi kuchukua Headlines.Huu ni mtihani sana na majibu yake Yatajulikana mwisho wa msimu baada ligi kuisha
Subscribe to:
Comments (Atom)


































