Thursday, 9 June 2016

Zlatan Ibramovich huwenda akawa Star wa tatu kusajiliwa na JoseMorinyo

       

Baada ya jana June 8 klabu ya Man United iliyopo chini ya Jose Mourinho kufanikiwa kufanya usajili wake wa kwanza kwa kunasa saini ya Eric Bailly kutoka Villerreal ya Hispania, leo June 9 2016 wameripotiwa kutenga kiasi cha pound milioni 47 ambazo ni zaidi ya bilioni 140 za kitanzania kwa ajili ya kuishawishi Juventus ya Italia iwauzie Alvaro Morata.

Tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa na wengi kuwa Zlatan Ibrahimovic ndio staa atakayefuatiwa kusajiliwa Man United baada ya Eric Bailly, lakini taarifa zimetoka kuwa Man United wanalazimika kuchelewesha usajili wa Zlatan hadi June 31 ili amalize mkataba wake rasmi na PSG, kwani akisaini wakati huu atalazimika kuilipa PSG kutokana na mkataba wake kuwa na kipengele cha uaminifu.

No comments:

Post a Comment