Monday, 9 May 2016

Dar es salaam Nauli za mabasi yaendayo kasi zatajwa


Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.

SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni tsh 650 na mwanafunzi 200.

Njia kuu+pembezoni nauli ni 800 na mwanafunzi 200 mfano njia kuu yaani kutoka Kimara mpaka kivukoni nauli itakuwa 650 na ukitoka mbezi mwisho mpaka kivukoni (hapo umechukua njia ya pembeni ukaunganisha na njia kuu) nauli itakua 800, ukitoka Morroco mpaka kariakoo au kivukoni nauli itakuwa 650 mwanafunzi 200.

Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.

Msimamizi wa mradi kutoka DART, Eng Ronald Lwakatare amesema……….>>>‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’

Thursday, 5 May 2016

About Me


kwa ufupi jina langu kamili Lukman soud Almas blog hii ni mali yngu ambayo namiliki  takriban miez 3 bado mpya. Nahitaj saport sna kutoka kwenu kwani bila nyie kufatilia habari toka kwa hii blog itakuwa si chochote kwangu. Naombeni saport ili tuweze fika mbali.
 INSTAGRAM NATUMIA  bizyluqdube
FACEBOOK  bizyluq
TWITER     bizyluqd



Wednesday, 4 May 2016

Mambo matatu aliongea Ronado baada mchezo kumaliza na kutinga Final UEFA

     

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa siku 15 bila kucheza mechi yoyote ya ushindani kwa Cristiano Ronaldo, Usiku wa May 4 2016 aliingia kwenye headlines baada ya kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Man City akitokea majeruhi na kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Ronaldo alinaswa katika interview baada ya mechi kumalizika lakini amekaririwa akiongelea mchezo na kueleza kuwa wao walicheza vizuri kuliko Man City, walitengeneza nafasi nyingi kuliko Man City, kuhusu majeruhi alisema anashangaa kwa watu wenye mashaka na fitnes yake kwani yeye yupo fiti.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu lakini nafikiria kuwa tulicheza vizuri zaidi ya Man City, licha ya kutotumia nafasi tulitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza na cha pili, kuhusu majeruhi mimi nipo sawa japokuwa watu wana mashaka na fitness yangu sijui kwa nini, fainali ya UEFA natoa aslimia 50 kwa 50 kwetu sisi kushinda au Atletico”

Uteuzi mwengine wa Rais Magufuli

          

Taarifa kutoka Ikulu May 04 2016 imeeleza kuhusu uteuzi alioufanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, Rais Magufuli amemteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dododoma  

Monday, 2 May 2016

Baada ya Daraja la kigamboni kuanza kutumika watumiaji wategemee hili



April 16 2016 ni siku ambayo wakazi wa kigamboni walianza kulitumia daraja la ‘Nyerere’ Kigamboni na baaadae Daraja la Nyerere ‘kigamboni’ lilifunguliwa rasmi April 19 2016 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John pombe Magufuli.

Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) David Mziray ameongelea uanzishwaji wa usafirishaji wa abiria kwa daladala kupitia daraja la Nyerere ‘Kigamboni’ Dar es salaam…

>>>‘tunaomba kuamasisha wamiliki wa mabasi kuja kupata leseni kwa ajili ya kutoa huduma ya Kigamboni kwenda mbagala rangitatu, kigamboni kwenda temeke, kigamboni- stesheni, sasa hivi njia hizo ziko wazi, tunaamasisha magari ambayo yanabeba abiria 27 na kuendelea, nauli zinaanzia 400 mpaka 450‘


Swansea yaichapa Liverpool



Swansea City imeitoa nishai Liverpool na kujihakikishia maisha kwenye Premier League ndani ya msimu ujao.

Andre Ayew alianza kutupia bao la kwanza kwa kichwa kabla ya goli linguine kutoka kwa Jack Cork na kuiweka Swansea mbele kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0.
                

Goli la Christian Benteke ililifufua matumani kwa Liverpool kipindi cha pili lakini la pili la Andre Ayew ambalo lilikuwa ni la tatu kwa upande wa Swansea lilimaliza matumaini ya Liverpool japo kuondoka na pointi moja kutoka uwanja wa ugenini.

Brad Smith kwa upane wa Liverpool alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano.
              

Matumaini ya Liverpool kufuzu kucheza Champions League yamebaki kuwa ni kutwaa taji la Europa League pekee.

Ushindi huo unamaana kubwa kwaSwansea ambao wamebakiza michezo miwili tu kabla ya ligi kumalizika, matokeo hayo yanawafanya wasalie nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi huku wakiweka gap la pointi 11 kati yao na Sunderland inayoshika nafasi ya tatu kutoka chini.

Mambo muhimu ya kufahamu

Andre Ayew amefunga magoli mawili kwenye mechi moja kwa mara ya kwanza tangu atue Swansea.Swansea imefurahia ushindi wake wanne mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwenye Premier League.Christian Benteke amefunga goli lake la 50 ndani ya Premier League.Swansea imefunga magoli matatu kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho 25 April, 2015, time Jack Cork kwa mara ya mwisho.Gylfi Sigurdssonamehusika kwenye magoli 41 ya Swansea ndani ya Premier League (amefunga magoli 25 na kutoa assists 16), magoli 10 zaidi ya mchezaji yeyote wa Swansea (Wilfried Bony ndiye anayefata akiwa kahusika kwenye magoli 31 wakati akiitumika klabu hiyo).

Mzee Majuto atangaza rasmi kusataafu Kuigiza

              

Siku ya kwanza ya May 2016 jina la Mzee Majuto limetajwa tena kwenye vichwa vya habari kuhusu kuacha kwake kuigiza, 
  Gwiji la sanaa ya maigizo nchini Amri Athmani aka Mzee Majuto ametangaza rasmi kustaafu kuigiza na kutumia muda wake kumtumikia mola wake. Majuto amekuwa akifanya sanaa hii ya maigizo kwa muda mrefu na alianza kupata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 90. 

Nisha sishtuki na head lines na sijawahi kuwa na Baraka

                   

Jina la kuzaliwa Salma Jabu ila umaarufu anajulikana kwa jina la Nisha. exclusive
           
          Kuna ripoti ziliandikwa kwamba ulikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji Baraka Da Prince na ukasema humjui kabisa? JIBU >>> ‘Sijawahi kuandika hicho kitu na huwa simuandiki mtu kwenye page yangu, sipendi kuhusisha maisha yangu binafsi na maswala ya kazi yangu kwenye mitandao, sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, wa kirafiki au wa aina yoyote na Baraka Da Prince’

Umeshawahi kuwazia chochote kuhusu spidi ndogo ya Bongo movie kwenda nje ya mipaka ya Tanzania?

JIBU >>> ‘Mimi na timu yangu tulikaa tukalitazama hilo pia kama unakumbuka miezi miwili iliyopita kuna picha ziliruka nikiwa na mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi, kuna kitu kikubwa kinakuja kitahusisha soko la Afrika Mashariki‘

Sasa hivi una umri wa miaka 27, una mtoto tayari?

JIBU >>> ‘Ninae mtoto wa kike ana umri wa miaka 11, nilimpata nikiwa na miaka 17…. mitihani ya kidunia inatokea kila mtu ana historia yake, nilijutia lakini unaizoea ile hali na kujifunza kupitia ulipokosea…  ni stori ya kusikitisha na nikiiongea itaniumiza nitaanza kulia lakini ni kitu kiliniathiri sana kisaikolojia’

wanawake muwe makini huyu inasadikika kafa gest jana Amelishwa sumu

                


Tukio limetokea Guest House Kimara Dar es salaam usiku wa May 1 2016 ambapo Mwanaume mmoja aliyeingia kwenye nyumba hiyo ya Wageni akiwa na Mwanamke, alikimbia kwa kusingizia kwenda dukani kununua vocha wakati Mwanamke huyo akikaribia kukata roho na hakurudi tena.

Wakati tunasubiri uchunguzi wa Polisi, mashuhuda kwenye eneo la tukio wamesema inavyoonekana Mwanamke huyo atakua kawekewa sumu kwenye chips alizokua anakula ndani ya chumba cha nyumba hiyo ya Wageni chips ambazo inadaiwa walitokanazo kwenye safari yao na kuja nazo Guest House.

Sunday, 1 May 2016

Nakupa Kikosi cha simba zidi ya Azam Leo hii May1 2016

                 

1.Vicent    Agban
2.Emery    Nimuboma
3.Mohammedi    Tshabalala
4.Juuko    Murshid
5.Novart   Lufunga
6.Justise   Majabvi
7.Awadh   Juma
8.Jonas   Mkude
9.Hamis   kiza
10.Dany    Lyanga
11.peter  Mwalyanzi

  Bench.
Peter   Manyika
Mohammedi   Fakhi
Hassani    Is-haka
Brian   Majwega
Mussa   Mgosi

Harmonize kufanya balaa Geita jana April30 2016

Msanii Harmonize chini ya usimamizi mzuri wa Diamond platnam jana kupiga bonge la show geita. Harmonize alisema" Baada ya kumaliza showa nilijarib kugusia wimbo wa msanii mwenzangu ambae npo nae kwenye campony moja ya WCb, kikweli inaonyesha jinsi gani watu wana miss kuona showa yake ya kwanza akiwa jukwaani na kibao chake cha HUKU KWETU Rayvany(Raymond) alisema Harmonize

Domayo aikosa Simba Kipre arejea.

                          
   kwa ufupi
Kiungo wa Azam Frank Domayo ataendele kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili kutokana na maumivu ya cha mguu, Lakini mshambuliaji Kipre ypo fiti kuivaa Simba leo

Memphis Depay aondoka Man United

winga mshambuliaji wa klabu ya Man united ya uingereza Memphis Depay jina  lake limeingia kwenye headlines tena baada kufanya kitendo ambacho huwenda kikawa na maana ya kuwashiria yeye kukosa furaha ndani ya Man united .Memphis amewashangaza wengi hususani mashabiki wake wa Man United wanao Mfollow katika acout yake ya  Instagram baada kuona wingi hyo kufuta picha zote  zinazo husu Man United ambazo aliwah ku post.

Jambazi sugu lakamatwa Posta wawili wakimbia....Noah yakamatwa

Kijana mmoja anae sadikika jambazi akamatwa jijini Dar se salaam maeneo ya posta ,baada kutaka kumtapeli mama mmoja anae fanya kazi tigo pesa. Mashahidi waliokuwepo kwenye eneo hilo wanasema alikuwa analengo la kutaka kuweka pesa kiasi cha shilingi elf5. wakati yule dada anahesabu pesa zake kwanza ndipo yule jambazi akakwapua na kukimbia kwenye gari aina ya Noah, na kumrushia mtu alie kuwepo nyuma ya hilo gari. Wakati mchezo unaendelea dereva akajianda kuwasha gari ndipo raia wakamchomoa dereva na kumpiga na yule alieiba pesa wakamkamata . kama unavyo ona kwenye pcha