Monday, 2 May 2016
Nisha sishtuki na head lines na sijawahi kuwa na Baraka
Jina la kuzaliwa Salma Jabu ila umaarufu anajulikana kwa jina la Nisha. exclusive
Kuna ripoti ziliandikwa kwamba ulikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji Baraka Da Prince na ukasema humjui kabisa? JIBU >>> ‘Sijawahi kuandika hicho kitu na huwa simuandiki mtu kwenye page yangu, sipendi kuhusisha maisha yangu binafsi na maswala ya kazi yangu kwenye mitandao, sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, wa kirafiki au wa aina yoyote na Baraka Da Prince’
Umeshawahi kuwazia chochote kuhusu spidi ndogo ya Bongo movie kwenda nje ya mipaka ya Tanzania?
JIBU >>> ‘Mimi na timu yangu tulikaa tukalitazama hilo pia kama unakumbuka miezi miwili iliyopita kuna picha ziliruka nikiwa na mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi, kuna kitu kikubwa kinakuja kitahusisha soko la Afrika Mashariki‘
Sasa hivi una umri wa miaka 27, una mtoto tayari?
JIBU >>> ‘Ninae mtoto wa kike ana umri wa miaka 11, nilimpata nikiwa na miaka 17…. mitihani ya kidunia inatokea kila mtu ana historia yake, nilijutia lakini unaizoea ile hali na kujifunza kupitia ulipokosea… ni stori ya kusikitisha na nikiiongea itaniumiza nitaanza kulia lakini ni kitu kiliniathiri sana kisaikolojia’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment