BizyLuq
Monday, 25 July 2016
Harmmer q kuachia mkwaju wake mpya kabisa leo Tue,july 26
Msaniii wa miondoka ya style nyingi ikiwemo Bongo fleva ,Mduara hata zile za Arabik style Kwa jina anajulikana Hammer q leo kachia kibao chake kipya kabisa chenye style ya tofaut na ngoma zake zote . Anahitaj sapport ya kutosha kutoka kwenu mashabiki - ngoma inaitwa Hatotokea by Hammer Q
Thursday, 9 June 2016
Zlatan Ibramovich huwenda akawa Star wa tatu kusajiliwa na JoseMorinyo
Baada ya jana June 8 klabu ya Man United iliyopo chini ya Jose Mourinho kufanikiwa kufanya usajili wake wa kwanza kwa kunasa saini ya Eric Bailly kutoka Villerreal ya Hispania, leo June 9 2016 wameripotiwa kutenga kiasi cha pound milioni 47 ambazo ni zaidi ya bilioni 140 za kitanzania kwa ajili ya kuishawishi Juventus ya Italia iwauzie Alvaro Morata.
Tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa na wengi kuwa Zlatan Ibrahimovic ndio staa atakayefuatiwa kusajiliwa Man United baada ya Eric Bailly, lakini taarifa zimetoka kuwa Man United wanalazimika kuchelewesha usajili wa Zlatan hadi June 31 ili amalize mkataba wake rasmi na PSG, kwani akisaini wakati huu atalazimika kuilipa PSG kutokana na mkataba wake kuwa na kipengele cha uaminifu.
Monday, 9 May 2016
Dar es salaam Nauli za mabasi yaendayo kasi zatajwa
Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni tsh 650 na mwanafunzi 200.
Njia kuu+pembezoni nauli ni 800 na mwanafunzi 200 mfano njia kuu yaani kutoka Kimara mpaka kivukoni nauli itakuwa 650 na ukitoka mbezi mwisho mpaka kivukoni (hapo umechukua njia ya pembeni ukaunganisha na njia kuu) nauli itakua 800, ukitoka Morroco mpaka kariakoo au kivukoni nauli itakuwa 650 mwanafunzi 200.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.
Msimamizi wa mradi kutoka DART, Eng Ronald Lwakatare amesema……….>>>‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’
Thursday, 5 May 2016
About Me
kwa ufupi jina langu kamili Lukman soud Almas blog hii ni mali yngu ambayo namiliki takriban miez 3 bado mpya. Nahitaj saport sna kutoka kwenu kwani bila nyie kufatilia habari toka kwa hii blog itakuwa si chochote kwangu. Naombeni saport ili tuweze fika mbali.
INSTAGRAM NATUMIA bizyluqdube
FACEBOOK bizyluq
TWITER bizyluqd
Wednesday, 4 May 2016
Mambo matatu aliongea Ronado baada mchezo kumaliza na kutinga Final UEFA
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa siku 15 bila kucheza mechi yoyote ya ushindani kwa Cristiano Ronaldo, Usiku wa May 4 2016 aliingia kwenye headlines baada ya kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Man City akitokea majeruhi na kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Ronaldo alinaswa katika interview baada ya mechi kumalizika lakini amekaririwa akiongelea mchezo na kueleza kuwa wao walicheza vizuri kuliko Man City, walitengeneza nafasi nyingi kuliko Man City, kuhusu majeruhi alisema anashangaa kwa watu wenye mashaka na fitnes yake kwani yeye yupo fiti.
“Ulikuwa ni mchezo mgumu lakini nafikiria kuwa tulicheza vizuri zaidi ya Man City, licha ya kutotumia nafasi tulitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza na cha pili, kuhusu majeruhi mimi nipo sawa japokuwa watu wana mashaka na fitness yangu sijui kwa nini, fainali ya UEFA natoa aslimia 50 kwa 50 kwetu sisi kushinda au Atletico”
Uteuzi mwengine wa Rais Magufuli
Taarifa kutoka Ikulu May 04 2016 imeeleza kuhusu uteuzi alioufanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, Rais Magufuli amemteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dododoma
Monday, 2 May 2016
Baada ya Daraja la kigamboni kuanza kutumika watumiaji wategemee hili
April 16 2016 ni siku ambayo wakazi wa kigamboni walianza kulitumia daraja la ‘Nyerere’ Kigamboni na baaadae Daraja la Nyerere ‘kigamboni’ lilifunguliwa rasmi April 19 2016 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John pombe Magufuli.
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) David Mziray ameongelea uanzishwaji wa usafirishaji wa abiria kwa daladala kupitia daraja la Nyerere ‘Kigamboni’ Dar es salaam…
>>>‘tunaomba kuamasisha wamiliki wa mabasi kuja kupata leseni kwa ajili ya kutoa huduma ya Kigamboni kwenda mbagala rangitatu, kigamboni kwenda temeke, kigamboni- stesheni, sasa hivi njia hizo ziko wazi, tunaamasisha magari ambayo yanabeba abiria 27 na kuendelea, nauli zinaanzia 400 mpaka 450‘
Subscribe to:
Comments (Atom)








